Magonjwa ambukizi kama COVID-19 yanaweza kuvuruga mazingira ambamo ukuaji na maendeleo ya mtoto
hutokea. Kuvurugika kwa familia, urafiki, utaratibu wa kila siku, na jamii kwa ujumla kunaweza kuwa na athari
mbaya kwa ustawi wa watoto, ukuaji, na uangalizi. Kwa kuongezea, hatua zinazotumiwa kuzuia na kudhibiti
kuenea kwa COVID-19 zinaweza kuweka watoto katika hatari za uangalizi. Hatua za majumbani, hatua za utumiaji
vifaa maalumu, kuanzisha karantini kwa kanda mbalimbali na hatua za kujitenga zinaweza kuathiri vibaya watoto